Kaunti za Siaya, Kisumu Zaongoza kwa Maambukizi Mapya ya COVID-19
Mnamo Alhamisi, Juni 17, Wizara ya Afya ilitangaza maambukizi 660 mapya ya COVID-19, na kiwango cha chanya kimefika asilimia 10.7% baada ya sampuli 6,176 kupimwa katika saa 24 zilizopita. Kulingana na Wizara ya afya idadi ya wagonjwa nchini Kenya imefika 177,282 kutokana na sampuli 1,887,636 zilizopimwa tangu mwezi Machi 2020 kisa cha kwanza kilipotua nchini.